Paulino Wanawilla Unago, Waziri wa Sheria wa Sudan Kusini amesema
kuwa, kiongozi wa waasi, Riek Machar, anapaswa kushtakiwa kwa kosa la
uhaini. Unago ameeleza kuwa, Machar ambaye ni makamu wa rais wa zamani
pamoja na watu wengine 6 anaoshirikiana nao wanapaswa kushitakiwa kwa
uhaini kwa sababu ya kushiriki kwao katika machafuko ya hivi karibuni
Sudan Kusini. Waziri wa Sheria wa Sudan Kusini ameongeza kuwa, mtu
yeyote anayekusudia kubadilisha serikali halali kwa mujibu wa katiba au
kuiangusha kwa mabavu, ametenda kosa la uhaini.
Mapigano hayo yaliyositishwa hivi karibuni yanahesabiwa kuwa mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu Sudan Kusini ilipojitenga na Sudan mwaka 2011. Takwimu zinaonyesha kwamba, maelfu ya raia waliuawa na zaidi ya watu nusu milioni kuwa wakimbizi kutokana na mapigano hayo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!