Theluthi mbili ya watu wote waliobakwa
nchini Liberia mwaka jana wa 2013 walikuwa ni watoto. Hayo yameelezwa na
serikali ya nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika. Wizara ya Jinsia na
Maendeleo ya Liberia imetangaza kuwa asilimia 65 ya kesi 1,002 za
ubakaji zilizoripotiwa mwaka jana zilikuwa za watoto wenye umri wa kati
ya miaka mitatu na kumi na nne. Taarifa ya Wizara ya Jinsia na Maendeleo
ya Liberia imesema, watoto kumi kutoka kaunti nane waliokuwa na umri
kati ya miaka mitatu na 14 walifariki dunia mwaka jana baada ya kubakwa.
Hii ni katika hali ambayo ni wabakaji 49
tu ndio walioweza kufikishwa mahakamani na kushtakiwa kati ya jumla ya
kesi za ubakaji 137 zilizoripotiwa mahakamani mwaka jana huko Liberia.
Wizara ya Jinsia na Maendeleo ya Liberia imesema kuwa idadi ya watenda
jinai hiyo ya ubakaji ingekuwa ya juu iwapo wazazi wa watoto wanaobakwa
wasingekuwa wakifikia maridhiano na kumaliza kesi hizo, kwa kuwa wengi
wa wabakaji huwa ni ndugu wa karibu au marafiki.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!