Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , » NCHI YA BURUNDI YAWEKEZA DOLA $25 KATIKA INTANETI YA KASI

NCHI YA BURUNDI YAWEKEZA DOLA $25 KATIKA INTANETI YA KASI

Written By Unknown on Wednesday, 22 January 2014 | Wednesday, January 22, 2014


Serikali ya Burundi imezindua mradi wa dola milioni 25 za Kimarekani kwa ajili ya mtandano wa Intaneti wenye kasi kubwa nchini humu.
Mradi huo umezinduliwa jana hupa Bujumbura na Rais Pierre Nkurunziza ambaye alisema mashirika manne binafsi na serikali ndio wamiliki wa mkongo wa taifa wa mawasiliano (fiber optic) wenye lengo la kuhakikisha wananchi wote wanapata Intaneti kwa bei nafuu ifikapo mwaka 2025. Tayari kebo ya mkongo huo wenye urefu wa kilomita 1,000 imeshawekwa katika mikoa 17 ya nchi.
Kebo hiyo itaunganishwa na kebo za chini ya bahari ambazo zinaunganisha Afrika na dunia nzima kupitia bandari za Mombasa, Kenya, na Dar-es-Salaam Tanzania.
Benki ya Dunia imefanya utafiti unaoonyesha kuwa kuimarika kwa asilimia 10 kasi Intaneti kunaweza kuongeza pointi asilimia 1.4 katika ustawi wa kiuchumi kila mwaka. Burundi ina idadi ya watu milioni 8 na kasi yake ya Intaneti iko chini sana ikilinagnishwa na nchi nyingine za eneo la mashariki mwa Afrika
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi