Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » SOMA HISTORIA YA SIKU KAMA YA LEO MYAKA KADHA ILIYO PITA

SOMA HISTORIA YA SIKU KAMA YA LEO MYAKA KADHA ILIYO PITA

Written By Unknown on Sunday, 12 January 2014 | Sunday, January 12, 2014

Siku kama ya leo miaka 50 iliyopita yaani sawa na mwaka 1964 Miladia, kulitokea mapinduzi visiwani Zanzibar na Sheikh Abeid Amani Karume aliyekuwa kiongozi wa Chama cha Afro Shiraz kwa kifupi ASP, akawa Rais wa kwanza wa visiwa hivyo. Mapinduzi hayo yaliuondoa utawala wa Kisultani. Si vibaya kuashiria kuwa, Zanzibar na Tanganyika ziliungana na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 26 Aprili mwaka 1964. Aidha uhuru wa Zanzibar ulipatikana mnamo tarehe 10 Desemba mwaka 1963. Zanzibar inaundwa na visiwa viwili vya Unguja na Pemba  huku zaidi ya asilimia 95 ya wakazi wake wakiwa ni Waislamu.
Siku kama ya leo miaka 1463 iliyopita sawa na miaka 28 kabla ya Hijra, Mtukufu Mtume Muhammad (saw) alimuoa Bibi Khadija binti Khuwailid (as). Bibi Khadija alikuwa mwanamke sharifu, mwenye imani na maarufu kwa ukarimu wake katika zama za ujahilia na alikuwa maarufu kwa lakabu ya "Twahira" kwa maana ya msafi na mtoharifu. Baada ya kufunga ndoa na Nabii Muhammad (saw) Bibi Khadija alikuwa msaidizi mkubwa na mwenzi wa mtukufu huyo katika hatua zote za maisha yake. Alisabilia kila kitu kwa ajili ya Uislamu na Mtume Muhammad (saw). Aidha Bibi Khadija (as) aliishi pamoja na Mtume kipindi cha miaka 25 na daima alikuwa mke mwema na mwenye kujitolea kwa mumewe Mtume Muhammad (saw) mbora wa walimwengu.
Siku kama ya leo miaka 1480 iliyopita alifariki dunia babu yake Mtume, Abdul Muttalib katika mji wa Makka. Mtukufu huyo alikuwa miongoni mwa wakuu wa kabila la Kuraish kabla ya kudhihiri Uislamu na alikuwa hodari mno katika fasihi ya lugha ya Kiarabu. Bwana Abdul Muttalib alikuwa msimamizi na mshika ufunguo wa nyumba tukufu ya al-Kaaba. Aidha babu huyo wa Mtume alikuwa akitayarisha chakula na maji kwa ajili ya watu wanaozuru nyumba hiyo ya Mwenyezi Mungu na kazi hiyo aliirithi kutoka kwa baba yake. Aliheshimu mno mikataba na ahadi zake na kwa sababu hiyo alikuwa na ushawishi mkubwa baina ya watu. Miongoni mwa watoto wa mtukufu huyo ni Abdullah, baba yake Mtume Muhamamd (saw) na Abu Twalib, baba yake Imam Ali bin Abi Twalib (as).
Na siku kama ya leo miaka 138 iliyopita, alizaliwa Jack London mwandishi mashuhuri wa nchini Marekani. Kwa miaka kadhaa Jack alifanya safari katika eneo la ncha ya Kaskazini na maeneo mengine na kupata bahati ya kufahamiana na koo na kaumu mbalimbali katika maeneo hayo sambamba na kubainisha taswira ya masuala hayo katika vitabu vyake.  Jack London aliishi kwa muda wa miaka 40 huku akijihusisha na kazi ya uandishi kwa muda wa miaka 18.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi