Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » WAPALESTINA KUTOITAMBUA ISRAEL KAMA NCHI YA KIYAHUDI

WAPALESTINA KUTOITAMBUA ISRAEL KAMA NCHI YA KIYAHUDI

Written By Unknown on Sunday, 12 January 2014 | Sunday, January 12, 2014

Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema kuwa hataitambua Israel kama nchi ya Kiyahudi.
Abbas alisema hayo jana akiwahutubia maelfu ya Wapalestina huko Ramallah katika Ukingo wa Magharibi na kuongeza kuwa, Wapalestina hawataacha takwa lao la kufanywa eneo la Quds Mashariki kuwa mji mkuu wa nchi huru ya Palestina. Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina aidha amesisitiza kuwa, hatakubali suluhisho lolote litakaloshindwa kufanikisha takwa hilo.
Wakati huo huo Catherine Ashton Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya amesema kuwa, vitongoji vya Israel vinavyojengwa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ni kinyume cha sheria na kikwazo kikuu cha kupatikana amani katika Mashariki ya Kati. Ashton pia ameutaka utawala wa Kizayuni wa Israel usitishe ujenzi wa vitongoji hivyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi