Sawarmi Khaled |
Sawarmi Khaled msemaji wa jeshi la nchi hiyo amesema, Januari 9 batalioni ya Nuer ilivuka mpaka katika eneo la Heglig na jeshi la Sudan liliwapokonya silaha waasi 54 na kuwapa hifadhi kama wakimbizi. Ameongeza kuwa, wale ambao walikataa kukabidhi silaha walirejeshwa Sudan Kusini.
Disemba 15 mwaka uliopita, mapigano yalianza kati ya vikosi vya serikali ya Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini anayetoka katika kabila la Dinka na askari watiifu kwa makamu wa zamani wa rais wa nchi hiyo Riek Machar anayetoka kabila la Nuer. Kundi la International Crisis linadai kuwa karibu watu 10,000 wameuawa na wengine wengi kuwa wakimbizi huko Sudan Kusini kwa sababu ya mapigano hayo.
Siku ya Ijumaa wapiganaji wa Machar walishindwa katika mji wa Bentiu na mji huo sasa unadhibitiwa na vikosi vya serikali.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!