Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » ULIMWENGU UNA MENGI,WACHINA WAO NDO WAANZA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA WA 2014(YEAR OF THE HORSE)

ULIMWENGU UNA MENGI,WACHINA WAO NDO WAANZA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA WA 2014(YEAR OF THE HORSE)

Written By Unknown on Thursday, 30 January 2014 | Thursday, January 30, 2014

 Wakati nchi nyingine duniani zikiwa zimeshaanza kusahau sherehe za kuukaribisha mwaka mpya 2014 zilizoanza na mkesha December 31, na kuadhimishwa rasmi January 1, 2014, wananchi wa China wao wanausubiri kwa hamu mwaka mpya ambao wataukaribisha rasmi January 31, mwaka huu.
Kwa mujibu wa kalenda hiyo, wanaanza ‘Year of the Horse’.
China inaukaribisha mwaka mpya kwa mujibu wa kalenda yao inayofuata mbalamwezi ‘Lunar Calendar’, na watasherehekea kwa takribani siku kumi na tano (hadi February 15). 

Kila siku ya sherehe hizo katika siku hizo kumi na tano inakuwa na ishara ama maana maalum kwa mujibu wa tamaduni za Kichina. Kwa mfano, siku ya tisa ni siku watakayoadhimisha kuzaliwa kwa mfalme wa mbingu, Jade Emperor, na Mungu wa utajiri/mali anaaminika kumwaga baraka zake katika siku ya tano ya sherehe hizo.
Watu mbalimbali kutoka nchi za jirani wameanza kuingia China kushuhudia sherehe hizo zinazoambatana na maonesho ya tamaduni za kichina, huku mapambo ya farasi na dragon yenye rangi nyekundu yakiwa yanatawala katika maeneo mbalimbali.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi