Hii ni vizuri kuifahamu mtu wangu wa nguvu wakati unasherehekea siku
hii ya Valentine na yule umpendaye ni vizuri kujua maana halisi ya hii
Valentine Day ambayo imeapishwa kufanyika kila mwaka February 14.
Neno Valentine lilitokana na jina ‘Valentino’ huyu alikuwa Mtakatifu
wa Kiroma aliyeitwa Valentino,siku ya Valentino hufahamika kama Siku ya
wapendanao na wengi wanaiita ‘Valentine Day’ ni maadhimisho ambayo
hufanyika kila mwaka.
Watu wengi husherehekea siku hii kwa kuonyesha upendo,kuthaminiana
pamoja na kujaliana kati ya watu wenye mahusiano mbalimbali ya karibu
japo mara nyingi siku hii hutumiwa na walio kwenye mahusiano ya
kimapenzi.
Valentine Day,asili ya Siku hii ni baada ya wakristo wa zamani
kuteswa hadi kufa kwa ajili ya kuupenda Ukristo na Kihistoria Mtakatifu
Valentino alitumika kama kiongozi wa dini kanisani katika utawala wa
mfalme Claudia.
Mfalme Claudia alimkamata na kumfunga,Mtakatifu Valentino aliteswa
kwa ajili ya Imani yake ya Kikristo na Kufa February 14 Kwa ajili ya
msimamo,imani yake na kufa kwa kutetea Ukristo Papa Gelasius aliitangaza
February 14 kuwa siku ya Mtakatifu Valentino mwaka 496 AD.
Katika siku hii kwako mtu wangu pengine kazi hua zinakubana kiasi cha
kukosa muda wa kuwasiliana mara kwa mara na ndugu wa karibu maana ni
vizuri kuwakumbuka na kuonyesha kuwa unawajali na kuwapenda,kama uko nao
mbali unaweza hata kuwapigia simu na kuwaeleza upendo wako kwao kama ni
baba/mama hata mlezi.
Pia si vibaya kuitumia siku hii kwa kujumuika na watu wenye kukosa
mahitaji muhimu au faraja kama watoto wanaoishi kwenye mazingira
magumu,Wagonjwa hata wazee wetu maana si lazima utoe pesa,lakini
ushiriki wako kwa chakula au mavazi unaweza kuwapatia,Happy Valentine
Day watu wangu wa nguvu.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!