Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko mashariki mwa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kimetangaza kuwa, watu zaidi ya sabini
waliuawa mwishoni mwa mwezi uliopita wa Januari na mapema mwezi huu
huko Congo Kinshasa kufuatia mashambulio ya waasi. Afisa mmoja wa Kikosi
cha kusimamia amani cha Umoja wa Mataifa MONUSCO amewaambia waandishi
wa habari mjini Goma kwamba, ndege ya wanajeshi wa UN, iliyokuwa
ikifanya uchunguzi katika eneo hilo, iligundua kuwa vijiji vitatu
viliteketezwa na kuharibiwa kabisa. Umoja wa Mataifa, umesema kuwa,
mauaji hayo yalitekelezwa na makundi ya waasi yaliyojihami katika mkoa
wa Kivu Kaskazini, ili kuzusha hofu baina ya watu wanaoishi katika eneo
hilo.
Martin Kobler, mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo ameelezea wasi wasi wake mkubwa alionao kutokana
na ukiukaji wa haki za binadamu katika nchi hiyo.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!