Miaka 51 iliyopita katika siku kama ya leo Martin Scott
tabibu mpasuaji wa Uingereza alifanikiwa kuunganisha figo ya mwanadamu.
Siku hiyo Prf. Scott alichukua figo ya mtu aliyekuwa amefariki dunia na
kuiunganisha na mgonjwa aliyekuwa amelazwa katika hospitali moja ya
Leeds huko Uingereza.
Na siku kama ya leo miaka 1369 iliyopita Mukhtar bin Abi
Ubaid Thaqafi alianza mapambano ya kulipiza kisasi cha damu ya Imam
Hussein bin Ali AS, mjukuu wa Mtume Mtukufu Muhammad SAW. Mwaka 61
Hijria Imam Hussein AS akiwa pamoja na wafuasi na watu wa familia yake,
aliuawa shahidi na jeshi la Yazid bin Muawiya kwenye vita visivyokuwa na
mlingano, kwa ajili ya kuilinda dini tukufu ya Kiislamu. Mukhtar
alianzisha harakati zake za mapambano katika mji wa Kufa. Kabla yake,
kulijitokeza kundi la 'Tawwabiin' ambalo lilitekeleza harakati dhidi ya
utawala wa Bani Umayyah, kwa lengo la kulipiza kisasi cha damu ya Imam
Hussein AS. Mukhtar Thaqafi alitawala Kufa kwa kipindi cha karibu mwaka
mmoja na mwishowe alishindwa na jeshi la Mus'ab bin Zubair na kuuawa.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!