BEKI, Mzambia Stopilla Sunzu amekuwa tishio Ufaransa baada ya
kutajwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Januari kwenye klabu ya Sochaux
inayoshiriki Ligi Kuu Ufaransa maarufu, Ligue 1.
Ikiwa ni mwezi wake wa kwanza tu kwenye ligi hiyo,
beki huyo wa kati ameonyesha ubora mkubwa na kuwafurahisha mashabiki wa
timu hiyo kutokana na staili yake ya uchezaji.
Kwenye mchakato huo, Stopilla, 24, aliwashinda
Sebastien Corchia na Jordan Ayew, ambao walishika nafasi ya pili na tatu
kwa ubora mwezi uliopita.
Tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea TP
Mazembe, staa huyo wa Chipolopolo amecheza mechi zote tano za
kiushindani, alifunga bao mwanzoni mwa mwezi huu kwenye mechi ya ushindi
dhidi ya Nantes.
“Stopilla Sunzu amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa
klabu hii kwa mwezi Januari baada ya kupata kura 26.2. Wengine
waliomfuatia ni Sebastien Corchia kura 23.7 na Jordan Ayew kura 13.4,”
ilibainisha taarifa kutoka tovuti ya Sochaux.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!