STAA mpya wa Manchester United, Juan Mata amedai atacheza katika
nafasi yoyote ambayo atapangwa na kocha wake, David Moyes, na ana
furaha kuamua kutua Manchester United kutoka Chelsea.
Jumatano usiku Mata alipangwa pembeni katika
pambano dhidi ya Arsenal, huku tayari Moyes alishamtumia nafasi ya
kiungo mchezeshaji nyuma ya mshambuliaji mmoja katika baadhi ya mechi
zilizopita.
Hata hivyo, Mata amedai kwamba hana tatizo na sehemu anayopangwa na atacheza eneo lolote ambalo Moyes ataamua kumpanga.
“Katika maisha yangu yote ya soka nimecheza
kushoto, kulia na hata nyuma ya mshambuliaji. Sijali kucheza popote
ambapo kocha ataniambia. Nina furaha klabuni hapa.
Nafurahia tena soka langu. Napata dakika nyingi za kucheza uwanjani,” alisema Mata.
“David de Gea amenisaidia kutulia. Chicharito,
Valencia na Rafael wote wanazungumza Kihispaniola, lakini kila mtu pia
amekuwa akinisaidia.”
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!