WINGA wa Bayern Munich, Franck Ribery, amefanyiwa operesheni ya
makalio na atakuwa nje ya uwanja mpaka Machi huku akitazamiwa kukosa
mechi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Arsenal.
Ribery anatazamiwa kuzikosa mechi tatu za Bayern
ikiwamo ya Jumatano ijayo dhidi ya Arsenal na kuna hatihati kama atawahi
pambano la marudiano litakalochezwa Ujerumani Machi 11.
Hata hivyo amepangiwa kurudi uwanjani Machi Mosi
katika pambano dhidi ya Schalke 04 ingawa haifahamiki kama atakuwapo
uwanjani siku hiyo au anaweza kuwa fiti kucheza na Arsenal siku 10
baadaye.
Mishipa ya damu katika makalio ya winga huyo wa
kimataifa wa Ufaransa, imepasuka na tayari upasuaji umefanyika kwa ajili
ya kuirekebisha. Tatizo hilo halitazamiwi kuwa la muda mrefu.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!