Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » SOMA HISTORIA AMBAZO ZINAAMBATANA NA SIKU KAMA YA LEO

SOMA HISTORIA AMBAZO ZINAAMBATANA NA SIKU KAMA YA LEO

Written By Unknown on Tuesday, 4 February 2014 | Tuesday, February 04, 2014

Miaka 35 iliyopita katika siku kama hii ya leo, katika hali ambayo mapambano ya wananchi wa Iran dhidi ya utawala wa Shah yalikuwa yamefikia kileleni baada ya Imam Ruhullah Khomeini kurejea nchini akitokea uhamishoni, Waziri Mkuu wa utawala wa kifalme wa Shah, Shapur Bakhtiyar alifanya jitihada za kuwatuliza wananchi bila ya mafanikio yoyote. Bakhtiyar alisema katika mahojiano na vyombo vya habari kwamba, angekabiliana vilivyo na maandamano hayo ya kidemokrasia na ya kudai uhuru na kwamba, hangemruhusu Imam Khomeini kuunda serikali ya mpito nchini. Wakati huo uasi wa kiraia, kukimbia wanajeshi na kujiunga na safu za wananchi katika miji mbalimbali ya Iran ikiwa ni pamoja na kujiuzulu wabunge, viongozi wa ngazi za juu serikalini na kadhalika kuliifanya serikali ishindwe kudhibiti hali ya mambo nchini.
Siku kama ya leo miaka 69 iliyopita, kulifanyika mkutano uliojulikana kwa jina la Yalta huko kusini mwa Urusi ya zamani kwa kuzishirikisha Uingereza, Marekani na Shirikisho la Urusi ya Zamani. Mkutano huo ulifanyika baada ya kudhihiri dalili za kushindwa Ujerumani katika Vita vya Pili vya Dunia. Lengo hasa la mkutano wa Yalta lilikuwa kujadili hali ya kisiasa na kijeshi ya nchi zilizokuwa zikipigana vita hivyo, ikiwa ni pamoja na kuainisha hatima ya ardhi zilizokuwa chini ya madola waitifaki.
Na siku kama ya leo miaka 1262 iliyopita, alizaliwa Sayyid Abdul Adhim al Hassani aliyekuwa mmoja wa wajukuu wa Imam Hassan al Mujtaba (a.s) huko katika mji wa Madina. Sayyid Abdul Adhim alikuwa mmoja kati ya shakhsiya walioaminiwa na Imam al Hadi (as) na alinukuu hadithi moja kwa moja kutoka kwa maimamu watukufu kama vile Ridha, Jawad na al Hadi (as).  Sayyid Abdul Adhim alihamia Iran kutokana na pendekezo la Imam al Hadi (as) kwa ajili ya kuwaongoza Waislamu na akaishi katika mji wa Rei karibu na Tehran ya sasa. Sayyid Abdul Adhim aliuawa shahidi mwezi Shawwal mwaka 250 Hijria.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi