Watu wasiopungua 70 wameuawa katika machafuko ya Jamhuri ya Afrika ya
Kati katika mapigano mapya kabisa yaliyoripotiwa kutokea nchini humo.
Kamishna wa Polisi Elie Mbailao amesema kuwa, machafuko hayo yamejiri
katika mji wa kati wa Boda ulioko umbali wa kilomita 100 kutoka mji mkuu
Bangui. Kamishna Mbailao amewaambia waandishi wa habari kwamba,
Wakristo waliokuwa na silaha waliwashambulia Waislamu katika mji huo na
kuchoma moto baadhi ya nyumba. Mauaji hayo yanatokea katika hali ambayo,
kuna maelfu ya wanajeshi wa Ufaransa na vikosi vya Kiafrika katika nchi
hiyo inayokabiliwa na machafuko. Ripoti zaidi kutoka nchini humo
zinasema kuwa, mashambulio dhidi ya Waislamu katika Jamhuri ya Afrika ya
Kati yameshadidi hasa katika mji mkuu Bangui, huku wafuasi wa dini hiyo
ambao ni wachache nchini humo wakiendelea kulengwa na mashambulio ya
kulipiza kisasi. Wanamgambo wa Kikristo wa Anti-Balaka wanawashambulia
Waislamu na hata kuchoma misikiti na mali zao ili kulipiza kisasi cha
mashambulizi ya huko nyuma ya waasi wa Seleka.
Home »
siasa afrika
» TAARIFA KUTOKA C.A.R ZASEMA KUWA WATU WAPATAO 70 WAMEFARIKI DUNIA
TAARIFA KUTOKA C.A.R ZASEMA KUWA WATU WAPATAO 70 WAMEFARIKI DUNIA
Written By Unknown on Tuesday, 4 February 2014 | Tuesday, February 04, 2014
Labels:
siasa afrika
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!