Serikali ya Sweden iliweza kusimamisha misaada ya kifedha iliyotengwa awali kwa
ajili ya serikali ya Uganda. Waziri wa Ushirikiano ya Maendeleo ya
Kimataifa amesema kuwa, uamuzi huo umechukuliwa kutokana na serikali ya
Uganda kupitisha sheria inayopiga marufuku vitendo vya liwati na usagaji
nchini humo. Bi. Hillevi Engstroem ameongeza kuwa, serikali ya
Stockholm inaunga mkono vitendo vya liwati na usagaji na itapeleka
misaada yake Uganda kupitia njia nyingine. Nchi nyingine za Ulaya kama
vile Denmark, Norway na Uholanzi tayari zimeshakata misaada yao kwa
serikali ya Uganda, na kuamua kutoa misaada hiyo kupitia taasisi na
sekta binafsi. Serikali ya Sweden ilitenga dola milioni 34 kwa serikali
ya Uganda, ambapo asilimia 42 ya fedha hizo zilipaswa kutumika katika
masuala ya kuboreshwa demokrasia, haki za binadamu na usawa wa kijinsia.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, sheria dhidi ya vitendo vya liwati na
usagaji ilipitishwa bungeni mwezi Disemba mwaka jana, na kutiwa saini na
Rais Yoweri Museveni tarehe 24 Februari mwaka huu, hatua ambayo
imekosolewa vikali na nchi za Magharibi.
Home »
siasa afrika
» JE,BAADA YA RAIS MUSEVENI KUPITISHA SHERIA INAYOPIGA MARUFUKU VITENDO VYA LIWATI NA USAGAJI ULIWAHI KUPATA TAARIFA ZAKUWA NCHI YA SWEEDEN ILIKATA NA YAO PIA MISAADA KWA NCHI HIYO?
JE,BAADA YA RAIS MUSEVENI KUPITISHA SHERIA INAYOPIGA MARUFUKU VITENDO VYA LIWATI NA USAGAJI ULIWAHI KUPATA TAARIFA ZAKUWA NCHI YA SWEEDEN ILIKATA NA YAO PIA MISAADA KWA NCHI HIYO?
Written By Unknown on Friday, 7 March 2014 | Friday, March 07, 2014
Labels:
siasa afrika
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!