Vyama vya siasa vya nchini Algeria
vimewataka wananchi wa nchi hiyo watumie vyema haki yao ya kupiga kura
na kutosusuia uchaguzi. Wawakilishi wa vyama 10 vya siasa na baadhi ya
taasisi za kiraia za Algeria leo wamesisitiza kuwa, kuna udharura wa
kushiriki kwa wingi wananchi katika upigaji kura kwani kususia uchaguzi
sio njia inayofaa kutumiwa kuleta mageuzi ya utawala nchini humo.
Vyama hivyo vimesema kuwa, kususia
uchaguzi kutatayarisha mazingira ya kufanyika udanganyifu. Kampeni za
uchaguzi wa rais wa Algeria zitaanza rasmi Machi 23 na uchaguzi huo
utafanyika April 17 mwaka huu. Kuna wagombea 12 waliojiandikisha
kugombea katika uchaguzi huo akiwemo rais wa sasa Abdulaziz Bouteflika.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!