Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » KITENDO CHAKUVUNJIWA HESHIMA QUR'ANI NCHINI MAURITANIA CHA LAANIWA NA CHAMA TAWALA CHA NCHINI HUMO

KITENDO CHAKUVUNJIWA HESHIMA QUR'ANI NCHINI MAURITANIA CHA LAANIWA NA CHAMA TAWALA CHA NCHINI HUMO

Written By Unknown on Friday, 7 March 2014 | Friday, March 07, 2014

Chama tawala cha Mauritania cha 'Umoja kwa Ajili ya Jamhuri' kimetoa taarifa ya kulaani kitendo cha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu, na kusema kuwa kitendo hicho ni dhambi isiyosameheka. Taarifa zinasema kuwa, watu wasiojulikana hivi karibuni walivamia msikiti mmoja kaskazini mwa mji mkuu wa Mauritania, Nouakchott na kuchana nakala za Qur'ani  Tukufu na kuzitupa ovyo. Viongozi wa chama tawala cha Mauritania wametaka waliotenda kitendo hicho wachukuliwe hatua kali.
Wakati huo huo makundi ya kisiasa na taasisi za kiraia za Mauritania yamepinga kitendo hicho cha kishenzi kwa kufanya maandamano. Vyombo vya habari vimetangaza kuwa, maandamano hayo ya kulalamikia kitendo cha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu yanaendelea katika mji mkuu Nouakchott na miji mingine ya Mauritania. Mwanzoni mwa mwezi Januari pia kulishuhudiwa tukio kama hilo katika eneo la kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
Kushatadi vitendo vya kupiga vita Uislamu nchini Mauritania kumepekea wizara inayoshughulikia masuala ya Kiislamu ya nchi hiyo iwatake maimamu wa Swala za Ijumaa walaani vitendo vya kuvunjiwa heshima matukufu ya Uislamu katika hotuba zao. Kuvunjiwa heshima matukufu ya Uislamu katika nchi kama Mauritania ambayo wananchi wake karibu wote ni Waislamu ni jambo la kushangaza. Baadhi ya wachambuzi wa mambo wanasema kuwa, vitendo kama hivyo vya kuvunjiwa heshima matukufu ya Uislamu nchini Mauritania vinatokana na kudhoofika uhusiano wa nchi hiyo na utawala wa Kizayuni wa Israel katika miaka ya hivi karibuni na pia njama za Wamagharibi. Kutokana na hisia za kupinga Uzayuni za wananchi wa Waislamu wa Mauritania, ni wazi kuwa miongoni mwa masuala yanayopewa kipaumbele na utawala wa Kizayuni na washirika wao wa Magharibi ni kudhoofisha dini hiyo ya Mwenyezi Mungu.
Weledi wa mambo wanasisitiza kwamba, harakati za mtandao wa kigaidi wa al Qaida katika nchi nyingi za Kiislamu za Afrika zinatekelezwa pia kwa lengo hilo na zinatumiwa kama kisingizio cha kuingilia masuala ya ndani ya nchi hizo. Katika nchi kama Misri, Sudan, Niger na Nigeria kunatekelezwa njama za kupinga Uislamu kwa kisingizio cha kuwaunga mkono Wakristo.
Kwa ujumla mwenendo wa mabadiliko unaoshuhudiwa hivi sasa barani Afrika unadhihirisha njama za siri za kuupiga vita Uislamu zinazotekelezwa na mabeberu katika bara hilo. Inaonekana kuwa, bara la Afrika hivi sasa linakabiliwa na njama mpya ambazo hazitaishia katika nchi chache. Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa, njia pekee ya kukabiliana na fitna hiyo ni kulinda mshikamano na Umoja wa Afrika uwe na nafasi yenye taathira katika kuzuia uingiliaji wa nchi za kigeni kwa kisingizio cha kutatua changamoto za bara hilo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi