Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema amesikitishwa na kushindwa
jumuiya za kimataifa kuutatua mgogoro unaoendelea kutokota nchini Syria
na kusisitiza kuwa, mapigano nchini humo ambayo yameingia mwaka wake wa
nne, yameitumbukiza nchi hiyo kwenye mgogoro mkubwa wa kiusalama na
kibinadamu. Ban Ki moon ameongeza kuwa, kila siku mamia ya raia wasio na
hatia huuawa nchini humo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amebainisha
kuwa, mwendelezo wa mapigano nchini humo umesababisha hadi sasa zaidi ya
watu laki moja na elfu thelathini kuuawa na mamilioni ya wengine
kuyakimbia makazi yao. Bila ya kuzitaja nchi zinazopeleka silaha kwa
makundi ya kigaidi nchini Syria, Ban Ki moon amesema kuwa, upelekwaji wa
silaha hizo kwa makundi ya kigaidi kumeshadidisha mgogoro huo.
Amesisitiza kuwa, jamii ya kimataifa haitafumbia macho kuona mgogoro huo
wa kibinadamu ukiendelea nchini Syria.
Home »
siasa kimataifa
» SOMA KILE ALICHO KISEMA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA MZEE BAN KI MOON KUHUSU INCHI YA SYRIA
SOMA KILE ALICHO KISEMA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA MZEE BAN KI MOON KUHUSU INCHI YA SYRIA
Written By Unknown on Thursday, 13 March 2014 | Thursday, March 13, 2014
Labels:
siasa kimataifa
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!