Mapigano makali yameanza tena baina ya Waislamu wa Madhehebu ya Maliki
na Ibadhi na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa na nyumba kadhaa
kuchomwa moto huko kusini mwa Algeria. Khadhwir bin Babaz mmoja wa
viongozi eneo hilo amesema kuwa, kikosi cha usalama cha Algeria
kimetumwa kusini mwa nchi hiyo kwa shabaha ya kuzuia mapigano hayo
yasisambae zaidi. Kiongozi huyo amesema kuwa, makumi ya watu
wamejeruhiwa na makumi ya magari yameteketezwa. Makundi hayo mawili
yaliwahi kupigana mwishoni mwa mwaka 2013 na kusababisha watu kadhaa
kujeruhiwa. Rais Abdulaziz Bouteflika wa Algeria ameiagiza Wizara ya
Mambo ya Ndani ya nchi hiyo kutafuta njia za kurejesha amani katika eneo
hilo. Wafuasi wa Madhehebu ya Maliki ni wachache huku Maibadhi wakiunda
asilimia kubwa ya waumini wa Kiislamu katika eneo la kusini mwa
Algeria.
Home »
siasa afrika
» TAARIFA KUTOKA ALGERIA ZASEMA KUWA HALI YA USALAMA KWA SASA SIO NZURI
TAARIFA KUTOKA ALGERIA ZASEMA KUWA HALI YA USALAMA KWA SASA SIO NZURI
Written By Unknown on Thursday, 13 March 2014 | Thursday, March 13, 2014
Labels:
siasa afrika
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!