Siku kama ya leo miaka 439,
ardhi ya Angola ilikaliwa kwa mabavu na mkoloni Mreno. Kabla ya Wareno
kuwasili Angola, ardhi hiyo ilikuwa sehemu ya utawala wa Kiafrika wa
Guinea. Baada ya Wareno kuidhibiti nchi hiyo walianzisha vituo vya
biashara katika maeneo yake yote ya pwani. Baada ya kumalizika vita vya
Pili vya Dunia, harakati kadhaa zilianzishwa nchini Angola kwa lengo la
kuipatia uhuru nchi hiyo. Hatimaye mwaka 1975 harakati za wapigania
uhuru zilizaa matunda baada ya nchi yao kupata uhuru.
Na Siku kama ya leo miaka 1375 iliyopita, alifariki dunia Muawiya bin Abi Sufiyan muasisi wa silsila ya Bani Umayya. Muawiya alizaliwa miaka 15 kabla ya Mtume Mtukufu kutoka Makka na kuelekea Madina, na aliingia kwenye dini ya Kiislamu baada ya Mtume Mtukufu SAW kuikomboa Makka. Muawiya alikuwa liwali wa Sham, baada ya Umar bin Khattab kuwa khalifa wa Waislamu. Wakati wa utawala wa Imam Ali AS, Muawiya bin Abi Sufiyan aliamua kuingia kwenye vita vya Siffin dhidi ya Imam Ali AS, kwa kisingizio eti cha kulipiza kisasi cha kuuawa Uthman bin Khaffan.
-------------------------------------------------------------------------------
Miaka 203 iliyopita na katika
siku kama ya leo kulinganana na kalenda ya Milaadia, nchi ya Paraguay
ilipata uhuru. Paraguay iligunduliwa katika karne ya 16 Miladia na
Muhispania mmoja na ikawa chini ya utawala wa Uhispania kwa zaidi ya
karne mbili. Baada ya uhuru nchi hiyo ilitawaliwa na serikali ya
kidikteta na kulishudiwa majaribio kadhaa ya mapinduzi na kila aliyekuja
madarakani aliongoza kidikteta. Uchaguzi wa kwanza huru wa Rais
ulifanyika nchini humo mwaka 1989. Kijiografia Jamhuri ya Paraguay
inapatikana huko Amerika Kusini baina ya nchi za Brazil, Argentina na
Bolivia.
-------------------------------------------------------------------------------Na Siku kama ya leo miaka 1375 iliyopita, alifariki dunia Muawiya bin Abi Sufiyan muasisi wa silsila ya Bani Umayya. Muawiya alizaliwa miaka 15 kabla ya Mtume Mtukufu kutoka Makka na kuelekea Madina, na aliingia kwenye dini ya Kiislamu baada ya Mtume Mtukufu SAW kuikomboa Makka. Muawiya alikuwa liwali wa Sham, baada ya Umar bin Khattab kuwa khalifa wa Waislamu. Wakati wa utawala wa Imam Ali AS, Muawiya bin Abi Sufiyan aliamua kuingia kwenye vita vya Siffin dhidi ya Imam Ali AS, kwa kisingizio eti cha kulipiza kisasi cha kuuawa Uthman bin Khaffan.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!