Mahakama ya Rufaa jijini
Nairobi, Kenya, imebatilisha uchaguzi wa Gavana wa jiji hilo, Dkt Evans
Kidero na kuagiza uchaguzi mdogo ufanyike. Mahakama imesema uchaguzi
uliompa ushindi Dkt. Kidero ulikumbwa na matatizo chungu nzima ukiwemo
uchakachuaji na ukiukwaji wa sheria za uchaguzi. Majaji wawili kati ya
watatu waliosikiliza kesi hiyo wamesema makosa yaliyojitokeza kwenye
uchaguzi huo yaliufanya ukose kufikia kiwango kinachohitajika kisheria
na hivyo kubatilisha matokeo yake. Hata hivyo jaji mmoja kwenye jopo
hilo amesema hakuona makosa makubwa kwenye uchaguzi huo uliompa ushindi
Bw. Kidero na hivyo kwa mtazamo wake amesema gavana huyo wa mji mkuu wa
Kenya alichaguliwa kihalali. Huko nyuma mahakama kuu ilikuwa imeamua
kwamba mwanasiasa huyo alichaguliwa kihalali. Mpinzani wake wa Karibu,
Ferdinand Waititu alikata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama kuu na
hatimaye rufaa yake imezaa matunda. Hata hivyo Kidero amesema atakwenda
katika mahakama ya kilele (Supreme Court) kupinga uamuzi wa majaji wa
mahakama ya rufaa.
Evans Kidero ni Gavana wa pili
kupoteza cheo chake wiki hii baada ya mwenzake wa jumbo la Embu, Martin
Wambora kutimuliwa na Bunge la Seneti kutokana na tuhuma za utumizi
mbaya wa mamlaka yake na ufujaji wa fedha za umma.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!