Serikali ya Angola itakuwa mwenyeji wa mikutano miwili itakayojadili hali inayoendelea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Taarifa zinasema kuwa, mikutano hiyo itakawashirikisha Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Afrika ya Kati na wale wa Ukanda wa Maziwa Makuu ya Afrika.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Angola imeeleza kuwa, lengo la kuitishwa mikutano hiyo ya siku mbili ni kuchunguza wa kina hali ya mambo katika maeneo ya mashariki mwa Kongo. Serikali ya Angola ni mwenyekiti wa mzunguko wa nchi wanachama wa Ukanda wa Maziwa Makuu ya Afrika. Inafaa kuashiria hapa kuwa, majimbo ya Kivu Kaskazini na Kusini yanakabiliwa na mapigano na machafuko kutokana na kuwepo harakati za makundi ya wanamgambo waasi katika maeneo hayo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!