Rais wa Uruguay José Mujica, amedhihirisha hasira zinazomkabili kwa sasa mara baada ya kuona timu yake ya taifa ikiondolewa kwenye fainali za kombe la dunia, zinazoendelea nchini Brazil, baada ya kufungwa na timu ya taifa ya Colombia mabao mawili kwa sifuri mwishoni mwa juma lililopita.
Mujica mwenye umri wa miaka 79, amedhihirisha hasira zake baada ya siku mbili kupita ambapo ilishuhudiwa vijana wake wakishindwa kufurukuta mbele ya Colombia na kukubali kutupwa nje ya fainali hizoa mbapo ilidhaniwa huenda Uruguay wangefika mbali.
Raisi huyo bado ameonyesha kuwa na kumbukumbu ya adhabu iliyomfika mshambuliaji Luis Suarez, na kuamini sakata hilo ndilo chanzo cha kikosi chake kupoteza muelekeo pindi walipokuwa wakipapatuana na Colombia.
Amesema hakubaliani na yoyote yule ambae anapinga kutokuwepo kwa Luis Suarez hakukusababisha Uruguay ifungwe na Colombia katika mchezo huo muhimu ambao ulikuwa unawavusha na kuwapeka kwenye hatua ya robo fainali endapo wangeshinda.
Hata hivyo José Mujica hakuishia kulaumu kuondolewa kwa kikosi chake, bali alidiriki kutoa matusi ya nguoni kwa maafisa wa shirikisho la soka duniani FIFA, kutokana na adhabu waliyompa Luis Suarez.
Mujica ameonekana katika picha za televisheni akisema ”Viongozi wa FIFA ni wapuuzi na hawana budi kuchukuliwa kama wahuni na wakati mwingine sitakosea kama nitawaita m-th-rf-ck-rs.”
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!