Naibu mwakilishi wa Libya katika Umoja wa Mataifa, amekiri kwamba makundi ya wabeba silaha ndiyo yanayoidhibiti nchi hiyo. Ibrahim Omar Dabbashi pia amesema kuwa, watu ambao wana ushawishi serikalini ndio wanaoyadhaminia mahitaji ya kifedha makundi hayo ya wabeba silaha. Huku akikosoa utendaji kongresi ya taifa ya nchi hiyo Addabash amesema kuwa yale yanayojiri nchini Libya hivi sasa yanatokana na uzembe wa taasisi hiyo pekee ya kutunga sheria na kusisitiza kuwa, Walibya wanatarajia kwamba bunge jipya la taifa hilo litaweza kuchukua hatua za maana katika kukabiliana na makundi yenye silaha nchini humo. Itakumbukwa kuwa uchaguzi wa bunge nchini Libya ulifanyika tarehe 25 mwezi huu wa Juni.
Uchaguzi ambao ulishuhudia ushiriki mdogo sana wa wananchi, hasa kutokana na baadhi ya makundi ya wabeba silaha kutishia kufanya mashambulizi dhidi ya vituo vya kupigia kura. Hivi sasa makundi ya wabeba silaha na wanamgambo ambao walishiriki katika mapinduzi ya ya mwaka 2011, wanafanya vitendo hivyo kama njia ya kuishinikiza serikali kuu. Aidha makundi hayo yanatumia maelfu ya silaha yalizo nazo kuendesha vitendo vya kikatili nchini Libya na kufanya njama za kuidhoofisha serikali ya Tripoli. Katika siku za hivi karibuni kumekuwa kukiripotiwa habari za watu wenye silaha kushambulia idara za serikali na kadhalika wanadiplomasia na raia wa kigeni nchini humo. Katika tukio jipya la hivi karibuni, watu wenye silaha, waliushambulia kwa silaha ya RPG, ubalozi wa Sudan mjini Tripoli. Kutekwa nyara raia wawili wa Uturuki katika mji mkuu wa nchi hiyo, ni miongoni mwa matukio mengine ambayo yameshuhudiwa katika siku za hivi karibuni nchini Libya. Matukio yote hayo yanajiri katika hali ambayo baadhi ya askari wa serikali wanashirikiana na makundi hayo ya wabeba silaha. Hivi sasa kuna mpasuko mkubwa ndani ya jeshi la Libya. Hii ni kwa kuwa baadhi ya askari hao wako chini ya serikali ya Tripoli, huku sehemu nyingine wakiwa chini ya uongozi wa Khalifa Haftar, jenerali msataafu wa jeshi la nchi hiyo. Haftar kwa kipindi cha mwezi mmoja na nusu na kwa kisingizio cha kukabiliana na makundi ya kigaidi yanayopigana dhidi ya serikali, amekuwa akiongoza operesheni pana za kijeshi mjini Benghazi mashariki mwa nchi hiyo. Nukta nyingine inayofaa kuzingatiwa ni kwamba, kwa muda mrefu Libya imekuwa ikikabiliwa na ongezeko la makundi ya kigaidi huku ikiwa ni moja ya lango kuu linalotumiwa na magaidi katika kufanya magendo ya silaha kuelekea maeneo mbalimbali ya dunia. Kwa upande mwingine eneo la mashariki mwa nchi hiyo ni moja ya maeneo ambayo yamegeuka kuwa mhimili mkuu wa machafuko. Tunaweza kusema kuwa, hivi sasa Libya inaelekea kwenye mustakbali uliogubikwa na giza totoro huku na ni vigumu kutabiri mustakbali wake utakuwa upi.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!