Kuna msemo wa Kiswahili uliozoeleka kuwa muwamba ngoma huvutia kwake. Wazungu wenyewe wanasema uzuri upo kwenye macho ya anaeangalia kitu hicho.
Baadhi ya mashabiki ambao hawaamini hayo yaliyoandikwa hapo juu wamemshambuli kwa kejeli mrembo Amber Rose baada ya kupost picha ya mpenzi wake rapper Wiz Khalifa kwenye Instagram na kumtaja kuwa mwanaume mwenye mvuto zaidi duniani.
“The sexiest man on Earth.” Aliandika Amber Rose.
Wengine walisema kuwa amewatukana wanaume kama Trey Songz.
“Speaking as a man and an inhabitant of earth I take offence to that statement." Aliandika shabiki mmoja anaetumia jina la deanxod.
Wengine waliandika comments zenye matusi pia.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!