Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , , , » MASHABIKI WA SOKA WA MAREKANII WAANZA KUMPA HESHIMA ZAIDI GOLI KIPA WAO TIM HOWARD,NAKUSEMA HUYU NI ZAIDI YA MLINDA LANGO.

MASHABIKI WA SOKA WA MAREKANII WAANZA KUMPA HESHIMA ZAIDI GOLI KIPA WAO TIM HOWARD,NAKUSEMA HUYU NI ZAIDI YA MLINDA LANGO.

Written By Unknown on Thursday, 3 July 2014 | Thursday, July 03, 2014

Mashabiki wa soka nchini Marekani wamempa thamani kubwa mlinda mlango wa timu yao ya taifa Tim Howard, baada ya kuonyesha ushujaa wakati wa mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya timu ya taifa ya Ubelgiji.
Mashabiki wa Marekani wamemuonyesha mlinda mlango huyo thamani kwa kuamini pamoja na kuokoa michomo kadhaa wakati wa mchezo dhidi ya Ubeljigi siku mbili zilizopita, bado wanaamini huenda akawa na uwezo wa kuzuia mambo mengine mengi ambayo yameshindikana duniani.
Kwa kuonyesha thamani kwa Tim Howard, mashabiki wa Marekani wametengeneza video maalum ambayo ni vimumu kufikirika lakini wao kwa upeo na thamani waliyompa mlinda mlango huyo ambaye pia anaitumikia klabu ya Everton ya nchini Uingereza wanaaminia anaweza kufanya hivyo.
Lakini picha za video hiyo zimetengenezwa kwa kutumia matukio mbalimbali ambayo yalifanywa na Tim Howard, akiwa kwenye majukumu ya kulinda lango wa kikosi cha Marekani.


Mbali na video hiyo mashabiki wa soka nchini Marekani wamethibitisha kuamini Tim Howard, ndiye mlinda mlango bora katika michuano ya kombe la dunia ya mwaka huu, licha ya kuonekana kwa walinda milango wengine kama Guillermo Ochoa (Mexico) pamoja na Vincent Enyeama (Nigeria).

Hizi ni picha za Howard wakionesha uwezo alio nao zaidi:



 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi