Mafuriko makubwa yaliyosababishwa na mvua nyingi zilizonyesha katika maeneo ya kusini mwa Brazil yamepelekea watu zaidi ya elfu 50 kuzihama nyumba zao. Hadi sasa watu elfu 40 wameondolewa katika jimbo la Santa Catarina kutokana na mafuriko makubwa yaliyoliathiri jimbo hilo. Katika jimbo la Rio Grande do Sul, watu 10,700 wamezihama nyumba zao baada ya kubomolewa na mafuriko.
Nyumba nyingi za maeneo ya kusini mwa Brazil yaliyotahiriwa na mafuriko zimezama kwenye maji. Jumla ya miji 37 imeakumbwa na mafuriko katika jimbo la Santa Catarina na mingine 59 katika jimbo la Rio Grande do Sul kusini mwa Brazil. Hali mbaya ya hewa imeyasabababishia majimbo hayo yaliyotajwa hasara ya dola milioni 233.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!