Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » HIZI NDIZO HISTORIA ZINAZO AMBATANA NA SIKU KAMA YA LEO YA IJUMAATATU JUNI 30.

HIZI NDIZO HISTORIA ZINAZO AMBATANA NA SIKU KAMA YA LEO YA IJUMAATATU JUNI 30.

Written By Unknown on Monday, 30 June 2014 | Monday, June 30, 2014


Siku kama ya leo miaka 54 iliyopita mwafaka na leo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Zaire) ilijitangazia uhuru wake na Joseph Kasavubu akawa rais wa nchi hiyo, huku Patrice Lumumba akiwa Waziri Mkuu. Kongo ilikoloniwa na Ubelgiji. Mapambano ya kudai uhuru yaliyoongozwa na Patrice Lumumba yalishika kasi katika miaka ya mwisho ya kumalizika kwa Vita vya Pili vya Dunia na kupelekea nchi hiyo kujipatia uhuru wake. Hata hivyo baada ya Kongo kupata uhuru zilianza harakati nyingi za uasi zilizokuwa zikiungwa mkono na Ubelgiji. Katika upande mwingine kulishadidi mapigano kati ya Lumumba na Musa Chumbe kiongozi aliyekuwa akiungwa mkono na Ubelgiji. Hatimaye mnamo mwaka 1965 Jenerali Mobutu Sese Seko aliyeungwa mkono na Marekani alifanya mapinduzi ya kijeshi na kutwaa madaraka ya nchi hiyo ambapo badaye alianza kuwakandamiza wananchi masikini wa Kongo.

******************************************************

Miaka 25 iliyopita na katika siku kama ya leo, Jenerali Omar Hassan Ahmad Al Bashir wa Sudan aliongoza mapinduzi ya kijeshi na kuuangusha utawala wa Swadiq Al Mahdi bila ya umwagaji damu. Utawala huo ulikuwa ukikabiliwa na matatizo mbali mbali ya ndani. Baada ya mapinduzi hayo Omar Hassan Al Bashir kwa kushirikiana na Hassan Al Turabi alianzisha chama cha Kongress ya Kitaifa huku yeye akiwa mwenyekiti wa chama hicho na rais wa nchi. Baada ya Al Bashir kutwaa urais alijitahidi kujitenga na siasa za Marekani, hatua ambayo iliipelekea serikali ya Washington kuichukia serikali ya Khartoum. Aidha hasira hizo za Marekani ziliifanya kuanzisha hatua za kiaduai dhidi ya serikali ya Al Bashir. Miongoni mwa hatua za kiadui zilizochukuliwa na Marekani dhidi ya Sudan, ni kuwaunga mkono waasi wa Kusini mwa Sudan ambapo mwaka 2011 eneo hilo la kusini lilijitenga na Sudan na kujitangazia uhuru wake.
****************************************************

Na katika siku kama ya leo miaka 23 iliyopita, mfumo wa utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini ulifikia tamati. Kuanzia mwaka 1948, weupe walio wachache nchini Afrika Kusini walianza kutekeleza siasa za kibaguzi nchini humo dhidi ya wazalendo weusi. Kwa mujibu wa siasa hizo, weupe walio wachache waliokuwa wakiunda asilimia 20 tu ya wananchi wa Afrika Kusini walihesabiwa kuwa jamii bora zaidi na iliyokuwa na nafasi muhimu katika uendeshaji wa masuala ya nchi hiyo. Sheria za kibaguzi kama vile za kupiga marufuku watu weusi kuoana na watu weupe na vilevile kushiriki katika harakati za kisiasa ni baadhi tu ya sheria za kibaguzi zilizotekelezwa na makaburu nchini Afrika Kusini. Siasa hizo ziliwakasirisha mno walimwengu na nchi nyingi duniani kukata uhusiano na utawala huo.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi