Katika hali ya kushangaza raisi wa klabu ya Zamalek ya nchini Misri
Mortada Mansour, ametangaza kufanya mazungumzo ya kumsajili aliyewahi
kuwa mchezaji bora wa dunia Ronaldo de Assis Moreira *Ronaldinho Gaucho*
ambae kwa sasa anaitumikia klabu ya Atlético Mineiro ya nchini kwao
Brazil.
Raisi wa Zamalek alitangaza mpango huo wakati akihojiwa kwenye kituo cha televisheni cha taifa cha nchini Misri, ambapo amesema anaamini watafanikiwa kukamilisha mpango wa kumsajili mshambuliaji huyo.
Hata hivyo mtangazaji Khaled Ghandour aliyekuwa anamuhoji Mortada Mansour, alionyesha kushangazwa na taarifa hizo na kujikuta akiuliza mara mbili mbili, lakini jibu aliloambulia kutoka kwa kingozi huyo lilikuwa la kushangaza pia.
Mortada Mansour alirejesha swali kwa mtangazaji huyo kwa kumuuliza kwa
nini anashangazwa na taarifa hizo, ama anataka kuona wanamsajili Barack
Obama?
Raisi wa Zamalek alitangaza mpango huo wakati akihojiwa kwenye kituo cha televisheni cha taifa cha nchini Misri, ambapo amesema anaamini watafanikiwa kukamilisha mpango wa kumsajili mshambuliaji huyo.
Hata hivyo mtangazaji Khaled Ghandour aliyekuwa anamuhoji Mortada Mansour, alionyesha kushangazwa na taarifa hizo na kujikuta akiuliza mara mbili mbili, lakini jibu aliloambulia kutoka kwa kingozi huyo lilikuwa la kushangaza pia.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!