
Muigizaji huyo wa 12 Years A Slave, ambaye ni mshindi wa tuzo ya Oscar ya mwaka jana kama muigizaji bora wa kike msaidizi, anaungana na wasanii wengine waliong’ara mwaka jana katika tasnia ya filamu pamoja na mwanamuziki Pharrell Williams kama members wapya wa Academy hiyo.
Wasanii wengine wenye umri mdogo watakaoungana na Lupita ni pamoja na Josh Hutcherson, Michael Fassbender, Ben Foster, Sally Hawakins, Julia Lousi-Dreyfus, Chris Rock na Jason Statham.
Rais wa Oscar Academy, Cheryl Boone Isaac ameeleza kuwa Academy ya mwaka huu itawahusisha watu ambao wana vipaji zaidi na wabunifu katika masuala ya fulamu.
“Mchango wao katika filamu umewaburudisha hadhira kote duniani, na tunajivunia kuwakaribisha kwenye Academy.” Aliseam Cheryl Boone.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!