Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » RAIS WA SHIRIKISHO LA SOKA LA URUGUAY AIPINGA ADHABU ALIYOPEWA MSHAMBULIAJI SUAREZ.

RAIS WA SHIRIKISHO LA SOKA LA URUGUAY AIPINGA ADHABU ALIYOPEWA MSHAMBULIAJI SUAREZ.

Written By Unknown on Friday, 27 June 2014 | Friday, June 27, 2014

Raisi wa shirikisho la soka nchini nchini Uruguay Wilmar Valdez, amesema atawasilisha rufaa ya kupinga adhabu iliyomuangukia mshambuliaji wa timu ya taifa ya nchi hiyo Luis Suarez ambayo iliyotolewa na shirikisho la soka duniani FIFA jana jioni.
Valdez, amesema hakuridhishwa na adhabu hiyo ambayo amedai ni kubwa mno kwa Suarez ukilingalisha na tuhuma zilizokuwa zinamkabili za kumng’ata beki wa timu ya taifa ya Italia Giorgio Chiellini, wakati wa mchezo wa mzunguuko wa tatu wa kundi la nne kwenye michuano ya fainali za kombe la dunia.
Valdez, amesema tayari ameshawagiza maafisa wa shirikisho la soka nchini Uruguay kuandaa rufaa hiyo na wakati wowote akuanzia hii leo itawasilishwa kabla ya muda wa kufanya hivyo haujafikia kikomo hapo kesho.
FIFA kupitia kamati ya nidhamu ilitangaza adhabu kwa Luis Suarez kwa kumfungia michezo tisa ambayo ipo chini ya shirikisho hilo la soka duniani kote, pamoja na kumtaka kutokujihusisha na masuala ya soka kwa kipindi cha miezi minne ikiwa ni pamoja na kuingia katika viwanja vya soka.
Mshambulaiji huyo pia ametozwa faini ya paund elfu 65,000.
Msemaji wa FIFA Rob Harris ndiye aliyepewa jukumu la kuwatangazia waandishi wa habari hukumu iliyochukuliwa dhidi ya Luis Suarez.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi