Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » JE,UMEZISOMA HIZI HISTORIA ZINAZO AMBATANA NA SIKU KAMA YA LEO IJUMAA YA JUNI 27?

JE,UMEZISOMA HIZI HISTORIA ZINAZO AMBATANA NA SIKU KAMA YA LEO IJUMAA YA JUNI 27?

Written By Unknown on Friday, 27 June 2014 | Friday, June 27, 2014

Tarehe 6 Tir miaka 33 iliyopita Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ambaye wakati huo alikuwa mwakilishi wa Imam Ruhullah Khomeini katika Baraza Kuu la Ulinzi na pia Imam wa Ijumaa wa Tehran, alinusurika jaribio la kutaka kumuua lililofanywa na wanachama wa kundi la kigaidi la MKO. Magaidi hao walilipua bomu katika moja ya misikiti ya Tehran ambako Ayatullah Khamenei alikuwa akihutubia hadhara ya watu na kumjeruhi vibaya. Hata hivyo Imam Khamenei aninusurika jaribio hilo kwa njia ya kimiujiza na baadaye akashika usukani wa kuongoza jahazi la Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran. Ayatullah Ali Khamenei alijeruhiwa vibaya mkono wake wa kulia katika shambulizi hilo.


-----------------------------------------------------------------------------------

Siku kama ya leo miaka 37 iliyopita Djibouti ilipata uhuru baada ya kukoloniwa kwa miaka kadhaa na serikali ya Ufaransa. Djibouti ilikuwa chini ya mkoloni Mfaransa tangu mwaka 1896 ikijulikana kwa jina la Somalia ya Ufaransa. Hata hivyo Djibouti hatimaye ilipata uhuru wake baada ya miongo minane ya mapambano. Djibouti ni miongoni mwa nchi za mwisho kujiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu.

 -----------------------------------------------------------------------

Na siku kama ya leo miaka 1216 iliyopita alifariki dunia faqihi, mtaalamu wa hadithi na mpokezi wa matukio ya kihistoria maarufu kwa jina la Abu Naiim. Alizaliwa mwaka 130 Hijria nchini Iraq na anatambulika kama mpokezi anayetegemewa na kuheshimiwa na maulamaa wa Kiislamu wa hadithi. Ameandika kitabu cha As Salaat na mwanahistoria maarufu Ibn Nadim anasema kuwa, msomi huyo ameandika pia vitabu vya "al Manasik" na "Masailul Fiqhi".
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi