Rais Obama akituliya kama maji mtunginii akiangaliya soka |
Obama, amezungumzia fainali hizo, baada ya kuishuhudia Marekani ikipokea kichapo cha bao moja kwa sifuri dhidi ya Ujerumani hapo jana, lakini bado The Stars and Stripes walifanikiwa kufuzu kucheza hatua inayofuata kufuatia matokeo ya mchezo wa Ureno dhidi ya Ghana.
Obama hapa na yeye ageuka kocha...aanza yake |
Obama, amesema amewaona wachezaji wa timu ya taifa ya Marekani wanacheza vizuri na sasa anaamini baada ya kufanikiwa kuvuka kwenye hatua ya makundi, watakuwa na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa dunia kwa mara ya kwanza.
Hata hivyo Obama amesema pamoja na kutarajia makubwa kutoka kwa wachezaji wake, bado hajapata nafasi ya kuzishuhudia timu nyingine zikicheza katika fainali hizo kama Uholanzi, Colombia, pamoja na Ufaransa.
Hapa Obama akihutubia kuhusiana na timu yake hiyo ya taifa:
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!