Home »
siasa afrika
» MWENYEKITI WA A.U BI ZUMA AONYA KWA MARA NYINGINE TENA KUHUSIANA NA VITENDO VYA KIGAIDI BARANI AFRICA.
MWENYEKITI WA A.U BI ZUMA AONYA KWA MARA NYINGINE TENA KUHUSIANA NA VITENDO VYA KIGAIDI BARANI AFRICA.
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Bi. Nkosazana Dlamini-Zuma
ameonya juu ya kuendelea vitendo vya kigaidi katika maeneo tofauti ya
bara la Afrika. Zuma aliyasema hayo jana katika mkutano wa viongozi wa
Umoja wa Afrika mjini Malabo, Equatorial Guinea na kuonya juu ya
kuendelea vitendo vya kigaidi katika nchi za Nigeria, Somalia na Kenya.
|
Bi. Nkosazana Dlamini-Zuma |
Bi. Zuma ameongeza kuwa, kuongezeka vitendo vya kigaidi katika nchi za
Kiafrika, kumeleta woga na wasi wasi mkubwa baina ya watu. Mkuu huyo wa
Kamisheni ya Umoja wa Afrika amesisitiza kuwa, kuzimwa sauti za silaha
katika nchi za Kiafrika, ni suala linalopaswa kupewa kipaumbele na kila
serikali. Katika kikao hicho cha hapo jana Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, Ban Ki moon, alisema kuwa, umoja huo utashirikiana bega kwa
bega na mataifa ya Afrika katika kukabiliana na migogoro na machafuko
barani humo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!