Wananchi wa Ufaransa wamefanya maandamano dhidi ya siasa za kubana
matumizi na kuipinga hadharani serikali ya Rais François Hollande wa
nchi hiyo. Maandamano hayo yalifanyika jana huko Paris mji mkuu wa nchi
hiyo. Matatizo ya kiuchumi nchini Ufaransa yanatajwa kuwa jinamizi
ambalo limezusha machafuko ya kijamii nchini nchini humo. Maandamano
kama hayo yamekuwa yakishuhudiwa pia katika miji mbalimbali ya nchi hiyo
ya Ulaya.
Kwa Mujibu wa ripoti hiyo, asilimia kubwa ya Wafaransa wanapinga mwenendo wa serikali ya Rais Hollande, suala ambalo limezusha maandamano ya wananchi katika miezi kadhaa ya hivi karibuni nchini humo. Kama hiyo haitoshi, kiwango cha kupendwa rais huyo kimepungua kwa asilimi 18. Kwengineko, Wizara ya Kazi ya Ufaransa imetangaza kuongezeka kiwango cha watu wasio na ajira nchini humo. Jana wizara hiyo ilitoa ripoti ambapo pamoja na mambo mengine ilieleza kuwa idadi ya watu wasio na ajira nchini humo imeongezeka mara dufu na kuleta wasiwasi mkubwa ndani ya mkoloni huyo mkongwe wa Ulaya.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!