Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » MASHAMBULIZI KADHAA YA HUKO MPEKETONI YANAYO DAIWA KUTEKELEZWA NA KUNDI LA AL-SHABAAB,SERIKALI YA SOMALIA YA YALAANI.

MASHAMBULIZI KADHAA YA HUKO MPEKETONI YANAYO DAIWA KUTEKELEZWA NA KUNDI LA AL-SHABAAB,SERIKALI YA SOMALIA YA YALAANI.

Written By Unknown on Tuesday, 17 June 2014 | Tuesday, June 17, 2014

Serikali ya Somalia imelaani vikali shambulio la kigaidi lililofanywa juzi usiku na kundi la ash Shabab katika eneo la Mpeketoni, lililoko Lamu  nchini Kenya. Abduweli Sheikh Ahmed Waziri Mkuu wa Somalia amesema kuwa, shambulio hilo la ash Shabab la Somalia nchini Kenya, halina lengo jingine isipokuwa kuua raia wasio na hatia.
Abduweli Sheikh Ahmed
Wakati huohuo, watu wasiopungua wanane wameuawa baada ya kundi la al Shabab kufanya shambulio jipya jana usiku nchini Kenya. Inafaa kuashiria hapa kuwa, wanamgambo wa ash Shabab wasiopungua 30 walilishambulia eneo la Mpeketoni, na kuwafyatulia risasi ovyo watu waliokuwa barabarani na mahotelini na kusababisha watu wasiopungua 48 kuuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa. Waziri wa Usalama wa Ndani nchini Kenya Joseph Ole Lenku amesema kuwa serikali ya Nairobi inafanya juhudi za kuwafuatilia magaidi hao na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria. Kwa upande mwingine, baadhi ya wabunge wanapanga mkakati wa kumsaili na hatimaye kumtimua Waziri Ole Lenku kwa tuhuma kwamba ameshindwa kukabiliana na mashambulio ya kigaidi.


TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi