Mazungumzo ya amani kati ya utawala wa Juba na upande wa waasi nchini Sudan Kusini, yameingia dosari baada ya pande zote mbili kususia mazungumzo ya jijini Addis Ababa kwa kile pande hizo zinadai ni matamshi ya kejeli yaliyotolewa dhidi yao.
Katibu mkuu wa jumuiya ya IGAD, Mahboub Maalim hapo jana amesema kuwa wakati wakiwa kwenye ukumbi wa mkutano, walipokea taarifa za pande hizo mbili kutokuwa tayari kushiriki mazungumzo, hatua ambayo ni pigo kwa wapatanishi hao, wiki moja tu baada ya rais Kiir na Riek Machar kukubaliana kuunda serikali ya mpito ndani ya siku 60.
Utawala wa Juba licha ya kutoeleza kwa kina sababu za wao kutotuma ujumbe wake kwenye mazungumzo hayo, umeeleza kupinga kauli iliyotolewa na katibu mkuu wa IGAD juma lililopita ambapo alidai “Itakuwa ni ujinga iwapo pande hizi mbili sinafikiri kuwa kila mmoja anaweza kupata ushindi kwa kutumia jeshi”Kuchelewa kwa mazungumzo haya kunafanya hali kuwa mbaya zaidi nchini humo kwakuwa ni miezi 6 sasa imepita toka kuzuka kwa mapigano ambayo yamesababisha mamia ya watu kupoteza maisha na wengine maelfu kuyakimbia makazi yao.
Katika hatua nyingine Umoja wa Mataifa umezionya pande hizo mbili dhidi ya kuendelea kuchelewesha kufanyika kwa mazungumzo haya ambayo ni muhimu kwa mustakabali taifa hili.
Waasi wa Sudan Kusini pamoja na Serikali ya Juba wameendelea kulumbana mara kwa mara licha ya mara kadhaa kutiliana saini mikataba ya kusitisha mapigano lakini wote kwa pamoja wameshindwa kutumiza ahadi zao.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!