Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , , » SIRI YAFICHUKAAA...HIZI NDO NCHI 4 ZA AFRICA AMBAZO AJENDA ZA SIRI ZA JESHI LA MAREKANIII ZIMEKAA,MUNGU IBARIKI AFRICA

SIRI YAFICHUKAAA...HIZI NDO NCHI 4 ZA AFRICA AMBAZO AJENDA ZA SIRI ZA JESHI LA MAREKANIII ZIMEKAA,MUNGU IBARIKI AFRICA

Written By Unknown on Monday, 2 June 2014 | Monday, June 02, 2014

Gazeti la Kimarekani la The New York Times limeelezea mipango ya siri ya muda mrefu ya Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo (Pentagon) katika nchi nne za Kiafrika ikiwemo Libya, Nigeria, Mauritania na Mali inayofanyika kwa kisingizio cha kutoa mafunzo maalumu ya kijeshi kwa majeshi ya nchi hizo. Tangu mwaka uliopita, Pentagon imekuwa ikitekeleza mipango yake maalumu na ya siri katika nchi hizo, mipango iliyoandaa mazingira ya kutumwa sehemu ya maafisa wa kijeshi wa Kimarekani katika nchi hizo. Taarifa ya Marekani kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Libya iliyosambaa katika vyombo vya habari katika siku za hivi karibuni, ni sehemu ya mipango hiyo ya siri. Gazeti hilo limeandika kuwa, lengo la kutekelezwa mpango huo ni kuimarisha mapambano dhidi ya kile kinachodaiwa kuwa ni mapambano dhidi ya mtandao wa al Qaeda barani Afrika na kutoa mafunzo kwa vikosi maalumu vya nchi hizo kwa lengo la kutumika pindi vikihitajika. Kudhoofika waitifaki wa Marekani barani Afrika katika mapambano dhidi ya al Qaeda, kumeisukuma Washington ifikirie njia za kutekeleza mkakati mpya wa kukabiliana na kundi hilo na hivyo kulazimika kutoa mafunzo kwa vikosi maalumu kwenye nchi hizo nne za Kiafrika. Moja kati ya malengo ya Marekani ni kutekeleza mpango wa kuweka kikosi hicho kwa lengo la kukabiliana na ugaidi katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Imeelezwa kwamba, kikosi hicho hakina uwezo wa kupambana na makundi ya wanamgambo kama vile Boko Haram nchini Nigeria. Hii ni katika hali ambayo, ripoti zilizotolewa zinaonyesha kuwa, mafunzo yatakayotolewa na jeshi la Marekani nchini Libya yatachukua muda wa miaka minane, na hii inaonyeha kuwa, vikosi vya Marekani vitakaa barani humo kwa muda mrefu zaidi kuliko ilivyoelezwa kwenye ripoti ya gazeti la New York Times. George W. Bush, Rais wa zamani wa Marekani alitoa amri ya kuundwa kikosi cha AFRICOM mwezi Oktoba 2007, na shughuli za kikosi hicho kuanza rasmi mwezi Oktoba 2008.
Kikosi hicho maalumu cha jeshi la Marekani 'Africom' barani Afrika kimeweka kambi yake Kelley Barracks katika mji wa Stuttgart nchini Ujerumani. Wakuu wa kiusalama na kijeshi wa Marekani wana mtazamo huu kwamba kuingia majeshi ya nchi hiyo barani Afrika, kutadhamini maslahi ya muda mrefu ya Washington katika kukabiliana na satua na ushawishi wa madola mengine yenye nguvu barani humo kama vile China. Viongozi hao wanaamini kwamba, bara la Afrika linabadilika na kuwa moja kati ya maeneo yenye kuzalisha makundi yenye misimamo ya kufurutu ada na ya kigaidi barani humo. Kwa hakika makundi kama vile Boko Haram na ash Shabab barani Afrika, yamezipa mwanya na fursa nchi za Magharibi kuingia kijeshi barani humo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi