Olusegun Obasanjo Rais wa zamani wa Nigeria amesema kuwa, mazungumzo ndiyo njia pekee itakayoweza kutatua mgogoro wa nchi hiyo changa barani Afrika. Umoja wa Afrika mwezi Machi uliunda kamati ya kuchunguza vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vilivyofanywa na majeshi na wanamgambo waasi huko Sudan Kusini.
Serikali ya Sudan ya Kusini ambayo ilijitenga na Sudan mwaka 2011, inakabiliwa na matatizo makubwa kama vile kuibuka uasi unaoongozwa na Riek Machar makamu wa zamani wa rais, balaa la njaa, nakisi ya bajeti ya serikali na mapigano katika majimbo ya Upper Nile, Unity na Jonglei yaliyoanza mwezi Disemba mwaka jana na kuendelea hadi sasa.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!