Viongozi wa nchi tano zenye uchumi unaokuwa kwa kasi duniani (BRICS) wameanzisha benki ya maendeleo kwa ajili ya kukabiliana na mfumo wa kifedha wa kimataifa unaodhibitiwa na nchi za Magharibi. Wakuu wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini wamechukua uamuzi huo katika mkutano wao uliofanyika huko Fortaleza nchini Brazil jana Jumanne.
Akizungumza katika mkutano huo, Rais Vladimir Putin wa Russia amesema kama ninavyomnukuu: "Bila ya shaka kuna njia madhubuti za kuzuia matatizo mapya ya kiuchumi duniani; na kwamba kuanzishwa benki hiyo pia kutaandaa msingi wa kujiri mabadiliko makubwa ya kiuchumi," mwisho wa kunukuu.
Rais wa Russia ametaka pia kuanzishwa taasisi mpya ya nishati ili kuzidisha usalama wa nishati kwa nchi wanachama wa kundi la Brics. Nchi za Brics zinaunda zaidi ya asilimia 40 ya jamii ya watu dunia.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!