Cole, ambaye alikuwa mchezaji wa klabu ya Chelsea kuanzia mwaka 2006 amesema aliamini soka lake lingeishia nchini Uingereza, lakini mambo yamebadilika na leo amejikuta yupo nje ya nyumbani.
Cole, amesema wakala wake ndio chanzo cha kukubali kuondoka jijini London na kwenda jijini Roma, kutokana na mambo mazuri aliyomueleza kufuatia ofa iliyokuwa mkononi mwake mara baada ya mkataba na Chelsea kufikia kikomo mwezi uliopita.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 33, ameongeza kuwa baada ya kupewa taarifa hizo, mipango mbalimbali ilifanywa na alivutiwa na ukarimu wa viongozi pamoja na wafanyakazi wa AS Roma baada ya kufanya nao mawasilino siku chache kabla ya kufanya maamuzi.
Amesema amewahi kukutana nalo mara kadhaa na ameona ni jambo ambalo haliwezi kumalizwa kwa mara moja, hata kama adhabu kali zitachukuliwa kwa wahusika ambalo siku zote wamekua hawapendezwi na watu wenye asili ya bara la Afrika.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!