Wakatio huo huo serikali ya Afrika Kusini imelaani mashambulio ya
utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza na kueleza
kuwa matukio ya hivi sasa huko Palestina hayapasi kuiathiri serikali ya
umoja wa kitaifa ya Palestina. Mbali na serikali ya Afrika Kusini, vyama
vingine vya nchi hiyo, navyo pia vimetoa taarifa kwa nyakati tofauti
vikilaani mashambulio ya utawala wa Kizayuni na kusisitiza juu ya
ulazima wa kuwaunga mkono raia wa Palestina wa Ukanda wa Ghaza.
Hii ni katika hali ambayo wanaharakati wanaowaunga mkono wananchi wa Palestina huko katika mji wa Pretoria nchini Afrika Kusini wamefanya maandamano na kutaka kufukuzwa balozi wa utawala wa Kizayuni nchini Afrika Kusini. Hadi sasa Wapalestina zaidi ya 190 wameshauliwa shahidi na wengine zaidi ya 1400 kujeruhiwa tangu kuanza mashambulio ya pande zote ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ghaza.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!