Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , , » TABIA YA UVUJISHAJI WA NYIMBO ZA WASANII NCHINI TANZANIA YASHIKA KASI,SASA IMEMKUMBA RICH MAVOKO NA WIMBO WAKE WA "TURURU" WAVUJA.

TABIA YA UVUJISHAJI WA NYIMBO ZA WASANII NCHINI TANZANIA YASHIKA KASI,SASA IMEMKUMBA RICH MAVOKO NA WIMBO WAKE WA "TURURU" WAVUJA.

Written By Unknown on Wednesday, 16 July 2014 | Wednesday, July 16, 2014

Rich Mavoko amekana kuachia wimbo mpya unaoitwa ‘Tururu’ wimbo ambao ulisambaa sana jana kwenye mitandao ya kijamii na websites na kupata namba nzuri ya watu walioupakuwa.
Akiongea na waandishi wa Habari, Rich Mavoko amesema binafsi ameshangaa  baaad aya kusikia kuwa ametoa wimbo mpya na kwamba wimbo huo sio wimbo mpya, ni wimbo aliourekodi miaka mitano iliyopita na hana mpango wa kuutoa.
“Sio ngoma mpya, cha kwanza nachoweza kusema. Si ngoma ambayo nimeitoa mimi. Yaani sijui nani ameileta, blog gani inafanya hivyo vitu. Kwa sababu ni ngoma ambayo nimeirekodi miaka mitano nyuma. Can you imagine ni ngoma ambayo nimeifanya hata kabla sijafanya Silali.” Rich Mavoko amasemaa.
Ameendelea kueleza kuwa hii sio mara ya kwanza watu kuvujisha nyimbo zake na yeye anaonekana kama anavujisha ngoma.
Mavoko amezungumzia pia mazingira ya kuvuja kwa wimbo huo ambao ameurekodi katika studio za Sharobaro Record chini ya producer Bob Junior.
“Sipendi kumlaumu producer wa hiyo kitu kwa sababu pia hata yeye anaweza kusema mimi nilikupa huyo wimbo. Kitu ambacho mimi nakumbuka mara ya mwisho huyo wimbo unakuja kuvuja..huu wimbo, nilishawahi kuwa na meneja hapo nyuma..sipendi kumuongelea. Nyimbo zangu nyingi baada ya kuachana na mameneja zinavuja yaani. Sipendi kumuongelea vibaya yeye lakini hii kitu inaniudhi.” Ameeleza.
Amesema kitu kinachomuumiza zaidi ni tofauti ya uwezo wake wa kuimba miaka mitano iliyopita unaosikika kwenye wimbo huo ambao ni tofauti kabisa na uwezo wake wa sasa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi