Wapalestina wengine sita wameuawa shahidi katika mashambulizi
yaliyoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni huko kaskazini na
mashariki mwa Ukanda wa Ghaza. Wapalestina hao wameuawa shahidi baada ya
ndege za jeshi la Israel kuzishambulia nyumba mbili za raia wa
Kipalestina kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza. Kijana mwingine wa
Kipalestina ameuliwa shahidi pia katika mashambulio ya ndege za utawala
wa Kizayuni katika eneo la al Zaitun huko Ghaza.
Kanali ya televisheni ya al Manar imezinukuu duru za kitiba na kuripoti kuwa, Mpalestina mwingine ameuawa shahidi katika mashambulizi ya ndege za kivita za utawala wa Kizayuni, mashariki mwa Ukanda wa Ghaza.
Katika kujibu mashambulio hayo yote ya Israel, wanamuqawama wa Palestina wamevurumisha makumi ya makombora na kuipiga mji mkuu wa utawala wa Kizayuni, Tel Aviv na vitongoji kadhaa vya walowezi wa Kizayuni na kusababisha hasara, vifo, na majeruhi.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!