Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , , » HUYU NDIE BINTI ALIYE TUMIA GHARAMA YA HALI NA MALI SHIDA YAKE AFANANEE TU NA MKE WA KANYE WEST AMBAE NI K.KARDASHIAN.

HUYU NDIE BINTI ALIYE TUMIA GHARAMA YA HALI NA MALI SHIDA YAKE AFANANEE TU NA MKE WA KANYE WEST AMBAE NI K.KARDASHIAN.

Written By Unknown on Wednesday, 16 July 2014 | Wednesday, July 16, 2014

Kupenda ama kutamani kuwa kama star fulani unaemkubali hakuna sheria ya mipaka zaidi ya mwenyewe kuthibiti hisia zako zisipitilize, lakini wapo wengine ambao wamechoka kutamani kuwa kama fulani na wameamua kutumia nguvu kuwa kama yeye.
Claire Leeson, msichana mwenye umri wa miaka 24, mkaazi wa Landani ametumia zaidi ya $30,000 (Tsh 49,755000)kufanya upasuaji ili afanane na Kim Kardashian.
Claire ameiambia This Morning kuwa aliamua kufanya hivyo kwa sababu alipokuwa shuleni wenzake walikuwa wanamcheka na kuuita ‘mbaya’ kuliko kitu chochote kilicho hai.
“Nilikuwa naambiwa kila siku mimi ndiye mbaya kuliko kitu chochote kilicho hai na kwamba inabidi nijiue. Nilipoacha shule marafiki zangu waliniambia kuwa ninavitu ambavyo vinafanana na Kim Kardashian.” Amesema Claire.
Ameeleza kuwa baada ya kuambiwa hivyo na marafiki zake aliamua kuanza kuangalia kwa makini Keeping Up With The Kardashians na akagundua kuwa kweli kuna vitu ambavyo wanafanana na Kim Kardashian.
“Tunafanana katika mabishano na vitu vingine. Nikafikiri ni mzuri sana na kwa kweli nilitaka kufanana nae.”

Hata hivyo, msichana huyo ambaye kwa kiasi fulani zoezi hilo limemuweka katika madeni amesema anaona alichokifanya kinathamani ya fedha aliyotoa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi