Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » GHARAMA ZA SANCHEZ ZAIFANYA JUVENTUS KUACHIA KAMBA,HUKU ARSENAL NA BARCELONA WAKIENDELEA KUMGOMBANIA.

GHARAMA ZA SANCHEZ ZAIFANYA JUVENTUS KUACHIA KAMBA,HUKU ARSENAL NA BARCELONA WAKIENDELEA KUMGOMBANIA.

Written By Unknown on Tuesday, 8 July 2014 | Tuesday, July 08, 2014


Vita na ubishi ni wapi mshambuliaji kutoka nchini Chile, Alexis Alejandro Sánchez atakapocheza soka lake mara baada ya kuthibitika ataachana na FC Barcelona katika kipindi hiki, huenda ikawa imemalizika kutokana na uongozi wa mabingwa wa soka nchini Italia Juventus kukiri hautoweza kumudu gharama za mchezaji huyo.
Viongozi wa klabu ya Juventus ambao walikua wakisubiriwa na viongozi wa FC Barcelona kuwasilisha ofa ambayo itakuwa zaidi ya paund million 32, wametoa taarifa hizo muda mcheche uliopita kupitia vyombo vya habari vya mjini Turin.
Taarifa hizo zinaipa nafasi klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza kubaki pekee kwenye vita ya kumuwania mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, kufuatia ofa ya paund million 32 ambayo waliiwasilisha huko Camp Nou tangu mwishoni mwa juma lililopita.
Kabla ya klabu ya Juventus kupewa nafasi ya kuwasilifa ofa yao kwa Sanchez, klabu ya Liverpool ilikuwa inatajwa katika mbio za usajili wa mchezaji huyo, kutokana na makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa FC Barcelona ambao wapo mbioni kukamilisha uhamisho wa Luis Suarez, lakini mambo yaligeuke dakika za mwisho.
Imeelezwa kwamba Alexis Sanchez hakuwa tayari kujiunga na klabu ya Liverpool na badala yake alionyesha nia ya kutaka kusajiliwa na Arsenal FC ya jijini London.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi