Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » HIKI NDICHO ILICHO KISEMA UMOJA WA MATAIFA YANI U.N KUHUSIANA NA WAASI WA F.D.L.R

HIKI NDICHO ILICHO KISEMA UMOJA WA MATAIFA YANI U.N KUHUSIANA NA WAASI WA F.D.L.R

Written By Unknown on Tuesday, 8 July 2014 | Tuesday, July 08, 2014


Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, una pia ruhusa ya kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya waasi wa Rwanda wa FDLR katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Abdullah Wafy, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kwamba, ili kuhakikisha waasi wa FDLR wanapokonywa silaha, umoja huo uko tayari kutumia hata nguvu za kijeshi. Ameongeza kuwa, mpango wa kukabidhi silaha kwa hiari hadi sasa haujawa na mafanikio makubwa kwani ni waasi 200 tu ndio waliokabidhi silaha zao kwa hiari. Abdullah Wafy amesisitiza kwamba, juhudi za kuwashawishi waasi hao wakabidhi silaha zao kwa hiari zinaendelea, lakini Umoja wa Mataifa umeweka pia chaguo la kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya waasi hao wa Kinyarwanda endapo mpango huo hautafanikiwa.
Duru za kisiasa zinaamini kwamba, Wakongo wanawaona waasi wa FDLR kuwa hawatishii amani katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo, lakini wanaamini kwamba serikali ya Rwanda haina azma thabiti ya kuwatokomeza waasi hao, kwani wanawatumia kama kisingizio cha kuingia kijeshi ndani ya ardhi ya Congo. Kuna karibu wanamgambo 2,000 wa kundi la FDLR la Rwanda ndani ya ardhi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi