Kuna tetesi kuwa Rihanna ambaye kwa muda mrefu kidogo amekuwa single baada ya kuachana na Drake amempata mpenzi mpya, rapper Big Sean.
Kwa mujibu wa mtandao maarufu wa udaku ‘MediaTakeout’, Rihanna na Big Sean walioenekana Jumamosi (July 5) wakiwa katika pool party a mchezaji wa NBA, Kevin Durant huko Los Angeles.
Mashuhuda walioeleza kuwa na uhakika walidai kuwa wasanii hao walifika katika eneo hilo kwa pamoja na walikaa na kuishi dakika zote kama couple.
Huyo hapo Big Sean akichonga na Rihanna kimya kimya...akimwambia ule C.Brown bado mtoto mdogo haijui thamani yako. |
Wakati Rihanna akiripotiwa kuanza maisha mapya ya mapenzi na Big Sean (kama ripoti ya media takeout itakuwa kweli), Chris Brown yeye anaripotiwa kuachana tena na Karrueche Tran ambaye huwa na maisha ya kuachana na kurudiana mara kwa mara.
“Love what you have before life teaches you to love what you lost.” Aliandika Karrueche Tran kwenye Instagram.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!