Makumi ya watu wameuawa katika mapigano mapya kati ya wanamgambo wanaobeba silaha huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Taarifa kutoka Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati zinasema kuwa, mapigano hayo yametokea katika kipindi hiki cha kukaribia safari ya siku mbili ya Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati. Taarifa iliyotolewa na Kikosi cha Kimataifa cha Kulinda Amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati MISCA kwa kifupi imeeleza kuwa, wanamgambo wa Kikristo wa Anti Balaka wamerusha guruneti msikitini mjini Bangui, wakati waumini wa dini ya Kiislamu wakifanya ibada katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Shambulio hilo limejeruhi watu kadhaa.
Wakati huohuo, kikao cha siku mbili cha kundi la kimataifa la mawasiliano kuhusiana na mgogoro wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kilianza shughuli zake jana huko Addis Ababa mji mkuu wa Ethiopia kwa lengo la kutafuta njia za kukwamua mgogoro wa nchi hiyo. Kikao hicho kinawashirikisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, mkuu wa mpango wa amani wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, mwakilishi kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika (ECOWAS), na Jenerali Noel Leonard Essongo ambaye ni mwakilishi wa Rais wa Jamhuri ya Kongo Brazzaville ambaye ndiye mpatanishi wa mgogoro wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!